Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kisesa na Waziri wa zamani wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina amehamia rasmi chama cha ACT Wazalendo leo Agosti 5, 2025.
Mpina ametambulishwa katika kurasa rasmi za mitandao ya kijamii ya ACT Wazalendo akiwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Dorothy Temu.
Uamuzi wa Mpina umekuja siku chache tu tangu jina lake lilipoachwa miongoni mwa walioteuliwa kuwania nafasi za ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).