Mrema apata jiko kwa milioni 4.2

HomeKitaifa

Mrema apata jiko kwa milioni 4.2

Mwenyekiti wa Tanzania Labour Party (TLP), Augustino Mrema leo Machi 24, 2022 amefunga pingu za maisha na mkewe Doreen Kimbi katika Parokia ya Uwomboni, Kiraracha mkoani Kilimanjaro.

Mremba (77) amewaambia waandishi wa habari kuwa anapaswa kulipa mahari ya shilingi milioni nne na laki mbili na ameshatoa milioni moja hadi sasa.

Ametaja moja ya sababu zilizomsukuma kuoa ni pamoja na kuepuka zinaa.

Kuhusu suala la umri, mke wa Mrema amesema yeye hajali na atazidi kumpendezesha mume wake ili arudi ujanani.

Septemba 2021, mke wa kwanza wa Mrema, Rose Mrema alifariki dunia.

error: Content is protected !!