Mshindi wa Tuzo ya Fasihi ya Nobel 2021 Prof. Abdulrazak Gurnah ameitikia wito wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi kufuatia heshima kubwa aliyoipatia Zanzibar na kurejea Tanzania ambapo wamefanya mazungumzo ya ana kwa ana.
Rais Mwinyi amempongeza Prof. Gurnah ambaye alifika Ikulu Zanzibar kufuatia mwaliko wa Rais na kumwambia kuwa Zanzibar inajivunia mafanikio yake na tuzo hiyo ya heshima aliyotunukiwa.
Dkt. Mwinyi amempongeza Profesa Gurnah kwa utayari wake wa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kkuleta maendeleo ikiwemo kuwepo kwa maonesho ya vitabu.
Profesa Gurnah alizaliwa mwaka 1948 chini ya uongozi wa Sultan na baadaye kuhamia Uingereza ambapo ameishi huko tangu 1960 na kufanikiwa kuwa profesa katika huo Kikuu cha Kent hadi alipostaafu hivi karibuni akifundisha Kiingereza na historia baada ya ukoloni.