Msichana: Epuka haya ukiwa mwezini

HomeElimu

Msichana: Epuka haya ukiwa mwezini

Ni kawaida kwa msichana kupata hedhi kila mwezi ambapo huambatana na mabadiliko mbalimbali ya mwili na wengi kupata maumivu makali.

Hivyo basi kuna baadhi ya vitu ambavyo unashuriwa kuviepuka ili usiweze kupata maumivu ukiwa kwenye hedhi.

Usile vyakula vyenye chumvi nyingi

Vyakula vilivyo na chumvi nyingi sio nzuri kwako wakati uko kwenye hedhi kwa sababu vinaweza kuzidisha maumivu ya tumbo lako. Zaidi ya hayo, inaweza kusababisha pia usiwe na furaha.

Usiache mlo wowote

Ukiwa hedhi hakikisha hauachi kula mlo wowote ule kwani kipindi hiki mwili wako unahitaji nguvu hivyo hakikisha unakula chakula kwa muda sahihi.

Epuka kunywa kahawa

Kahawa inaongeza maumivu hivyo ukiwa kwenye hedhi usinywe kabisa kahawa ili usipate hadha hiyo.

Badilisha taulo za kike

Usivae taulo za kike siku nzima bali hakikisha ubadilisha baada ya muda wa angalau saa 6 kwani ukivaa siku nzima itatengeneza harufu mbaya.

Epuka ngono zembe

Hakikisha una epuka kushiriki ngono zembe ukiwa kwenye hedhi hasa kama haupo tayari kuanzisha familia.

Unaweza kushiriki tendo la ndoa lakini hakikisha unatumia kinga.

 

error: Content is protected !!