Mtoto huyu aweka rekodi ya kuzaliwa na uzito mdogo zaidi duniani

HomeKimataifa

Mtoto huyu aweka rekodi ya kuzaliwa na uzito mdogo zaidi duniani

Mwaka 2020 huko Birmingham, Alabama nchini Marekani alizaliwa mtoto akiwa na wiki 21 tu  na uzito gramu 420. Kwa kawaida mtoto huzaliwa baada ya wiki 40, kwa maana hiyo ni kwamba mtoto huyo kwa jina Curtis alizaliwa kukiwa na upungufu wa wiki 19.

Mama yake Michelle Butler, alikwenda chumba cha kujifungulia tarehe 4 Julai, ambayo ni siku adhimu kabisa ya Wamarekani kuadhimisha siku ya Uhuru wa Taifa lao. Mama huyo bahati nzuri alijifungua pacha, Curtic na C’Asya ambapo C’Asya alifariki siku ya pili. Kwa mujibu wa madaktari, Curtis alikuwa na chini ya 1% ya kuishi, lakini ajabu ni kwamba Curtis alitoka mahatuti hadi hivi leo ana miezi 16 ya kuishi duniani akiwa na afya njema.

Curtis alikaa kwenye mashine maalumu ya kumsaidia kupumua kwa miezi mitatu, na mwezi wa nne 2021 alitoka hospitali baada ya siku 275 . Curtis amevunja rekodi rekodi iliyokuwa inashikiliwa na mtoto Richard Hutchinson alizaliwa na na wiki 21 na siku mbili, Rekodi ya Richard ilidumu kwa miaka 34, huku kabla yake kulikuwa na mtoto kutoka Canada alizaliwa na wiki 21 na siku tano.

error: Content is protected !!