Kunyoa kipara kwa mwanamke ni uamuzi wa kijasiri sana kwani inafahamika kwamba nywele ni moja ya urembo kwa mwanamke yoyote yule.
Lakini inabidi utambue mambo kadhaa kabla hujachukua uamuzi wa kunyoa kipara ili usije ukajutia baadae hivyo mambo haya 5 kabla hujachukua hatua.
Angalia umbo la kichwa chako
Kabla hujachukua maamuzi ya kunyoa kipara angalia kama umbo la kichwa chako kitaruhusu muonekano huo mpya au unaweza kuwajulisha baadhi ya marafiki juu ya umauzi wako huo.
Watu watakushangaa
Tambua kwamba watu wanaokuzunguka watakushangaa ukiwa kwenye muonekano huo mpya. Lazima hii itokee kwani hawajazoea kuona ukiwa na kipara.
Unaweza kujinyoa nyumbani
Kama utakua unaona aibu kwenye saluni kwa kinyozi kunyoa basi unaweza kujinyoa ukiwa nyumbani kwako. Lakini hakikisha unavifaa vinavyohitajika na pia kama utahitaji msaada muombe mtu wako wa karibu ili usijikate.
Kichwa chako kinahitaji matunzo
Unaponyoa kipara unakuwa umepunguza gharama ya kusuka na pia muda wakukaa bafuni wakati wa kuoga lakini bado kichwa kitahitaji matunzo hata kama hakina nywele. Utembeapo juani hakikisha unapaka mafuta yatakayokusaidia usiungue na miyonzi ya jua.
Baridi ni adui yako
Kumbuka kwamba kipindi cha baridi unapata shida sana kwahiyo unashauriwa kununua kofia au kuvaa masweta yenye kofia ili uweze kujikinga.