Mwendokasi Gerezani- Mbagala kuanza Novemba mwaka huu

HomeKitaifa

Mwendokasi Gerezani- Mbagala kuanza Novemba mwaka huu

Huduma ya usafiri wa mabasi yaendayo haraka maarufu mwendokasi katika njia ya Gerezani hadi Mbagala, jijini Dar es Saalam, unatarajiwa kuanza Novemba mwaka huu.

Baada ya ukamilishaji wa kuweka taa, mabasi yataanza rasmi katika njia hiyo ya Gerezani hadi Mbagala.

Hayo yamesemwa na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi yaendayo Haraka (DART), Dk. Athuman Kihamia na kuongeza kuwa mabasi yanaendelea kutengenezwa hivyo hadi Novemba mwaka huu yatakuwa yamekamilika na kuanza kutoa huduma hiyo kwa wakati.

Aidha, kuhusu changamoto ya upungufu wa magari ya mwendokasi katika njia ya Kimara hadi Gerezani na Kivukoni, Dk. Athuman alisema hadi Novemba mwaka huu magari 177 mapya yanatarajiwa kuanza kutumika, kutatua changamoto hizo.

error: Content is protected !!