Nauli 700

HomeBiashara

Nauli 700

Bei ya nauli ya bajaji za kuchangia mkoani Mbeya zimepanda hadi kufikia 700 baada ya bei hiyo kudumu kwa miaka tisa sasa.

Akizungumza na Nipashe, Mwenyekiti wa Umoja wa Madereva Bajaji Jiji la Mbeya, Feso Mwasimba amesema kupanda huko kwa bei hakujasababishwa na kupanda kwa bei za mafuta  bali kudumu kwa muda mrefu kwa kiwango hicho hicho cha nauli huku bajaji ikiwa ni usafiri ya kukodisha.

Ameeleza kuwa kiwango kitapanda kwa wanafunzi pia. Wale wa shule za msingi watalipa 200, sekondari 300 na watu wa zima kutoka 500 hadi 700.

“Bajaji ni chombo cha kukodiwa na abiria sio sawa na daladala ambazo wanapangiwa nauli na Latra. Madereva bajaji wanalalamikia sana nauli ya shilingi 500 kila mwaka pasipo kupandishwa,” ameeleza Mwasimba.

Badhi ya madereva wa bajaji wamesema kiwango hicho bado ni kidogo kwani wangetegemea nauli ipande hadi Tsh 1,000 ili nao wapate Maslahi.

Ofisa Mfawidhi wa Latra, Kanda ya Nyanda za Juu, Denis Daudi amesema hana taarifa za kupanda kwa nauli za bajaji na hivyo atafuatilia kwa kiongozi wa bajaji mkoa.

 

error: Content is protected !!