Wadau wa Sekta ya Usafiri Ardhini (Latra) imependekeza kupanda kwa nauli kutoka 450 mpaka 900 kwa kila kilomita ambapo Mamlaka ya uthibiti wa Usafiri Ardhini wapo katika mapitio ya pendekezo hilo.
Mkurugenzi Mkuu Latra,Gilliard Ngewe alisema wamefanya marekebisho hayo kwenye nauli za usafiri, ili kuwezesha kutekeleza shughuli zao kwa faida.
“Uwepo wa watoa huduma hizo umefanya upatikanaji wa usafiri kuwa rahisi na nafuu kwa wananchi, huku madereva wanaofanya kazi hizo,” alisema Ngewe.
Aidha madareva wa huduma za mtandao, Uber na Bolt walitoa wito kwa mamlaka kupandisha bei ili iwasaidie kuendesha biashara hizo huku wakieleza kwa sasa wanapitia maumivu ya kupata hasara.
“Ni ngumu. Unampeleka mtu anakulipa Sh 3000 na umetumia lita moja ya mafuta ambayo ni Sh2,630 na wakati huo unakata asilimia 15 ya wenye mtandao,” alisema Samson John, dereva wa Uber.