Nauli mpya za mabasi

HomeKitaifa

Nauli mpya za mabasi

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Ardhini (LATRA), Gilliard Ngewe amesema mchakato wa kukusanya maoni kuhusu nauli mpya za mabasi ya abiria ya mikoani utakamilika na maamuzi kutangazwa kabla ya mwisho wa mwezi huu Aprili. 

Ngewe alisema mabasi mengi yamekuwa yakitoza kiwango cha chini cha nauli zilizopangwa na Latra kwa sababu ya ushindani kwenye soko lakini sasa wanatumia kiwango kilichowekwa na mamlaka hiyo.

“Najua mabasi mengi yalikuwa yakiendeshwa chini ya bei ilikuwa imeshapangwa, lakini mabasi mengine mfano kama basi linaloenda Dodoma bei ilikuwa ni shilingi 24,100 ila yapo mabasi yalikuwa yakichukua ni shilingi 20,000 na kwa sasa kama yameanza kutoza shilingi 25,000 basi hapo ina maana yameongeza shilingi 900 na sio 5,000,” alibainisha.

Aidha, Ngewe alisema kati ya sababu zilizowabana wamiliki wa mabasi ilikuwa ni kwa nini wamekuwa wakitoza nauli chini ya kiwango kilichopangwa na sasa wanataka kiongezwe.

error: Content is protected !!