Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema serikali itaendelea kukuza sekta ya madini katika Mkoa wa Ruvuma kwa kujenga kongani ya viwanda inayohusiana na madini, kwani mkoa huo una bahati ya upatikanaji wa rasilimali hiyo.
Dkt. Samia amesema, serikali yake itatenga maeneo maalumu ya wachimbaji wadogo wa madini katika Wilaya za Tunduru na Nyasa na kuwajengea masoko ya madini ambapo atahakikisha uwepo wa upatikanaji wa zana za kisasa za uchimbaji wa madini hayo.
Mgombea huyo, amesema hayo leo Septemba 22, 2025, wakati akinadi sera za CCM Songea Mjini mkoani Ruvuma kuelelekea uchaguzi mkuu, utakaofanyika mwezi Oktoba mwaka huu.