Rais Samia afanya uteuzi

HomeKitaifa

Rais Samia afanya uteuzi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokt. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa Makatibu wakuu wawili, kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa leo na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya rais Ikulu, Zuhura Yunus.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa, Rais Dkt. Samia amemteua Dokta Hashil Twaib Abdallah kuwa Katibu mkuu Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara, na amemteua Bwana Kaspar Mmuya kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya ndani ya Nchi, uteuzi ambao umeanzia Disemba 9 mwaka huu, 2022.

Dkt. Hashil Twaib Abdallah

Kaspar Mmuya

error: Content is protected !!