Rais Samia aidhinisha shilingi bilioni 30 kukarabati barabara zilizoathiriwa na mvua

HomeKitaifa

Rais Samia aidhinisha shilingi bilioni 30 kukarabati barabara zilizoathiriwa na mvua

Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imepanga kutumia kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni 30 kwa ajili ya ukarabati wa barabara muhimu za maeneo mbalimbali nchini zilizoharibiwa na mvua.

Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega, ametoa taarifa hiyo mkoani Morogoro alikoenda kwa dharura baada ya mvua kubwa zinazoendelea kunyesha kuharibu barabara inayounganisha Ifakara – Mlimba kwenda mkoa wa Njombe.

Ulega alisema pamoja na kiasi hicho cha fedha kilichoidhinishwa na Rais kwa ajili ya ujenzi wa dharura, mipango ya serikali ya ujenzi wa kudumu wa barabara na madaraja inaendelea kama ilivyo na haiathiriwi na mipango hii ya dharura.

“Nimekuja kwenu wananchi wa Morogoro – na hasa nyinyi wa Ifakara, Malinyi, Ulanga na Mlimba, kuwafikishia salamu za Rais wenu na pole zake kwa taabu hii mliyoipata. Lakini nimekuja pia na habari njema.

“Rais wenu, Samia Suluhu Hassan, amekubali matumizi ya zaidi ya shilingi bilioni 30 kwa ajili ya ujenzi wa dharura wa barabara na madaraja yaliyoharibiwa na mvua hizi zinazoendelea, hapa kwenu na maeneo mengine ya Tanzania, ili maisha yenu yaendelee. Barabara ni uchumi. Barabara ni maisha na lazima kazi ziendelee,” alisema.

error: Content is protected !!