Rais Samia aikumbuka kata ya Kitandililo

HomeKitaifa

Rais Samia aikumbuka kata ya Kitandililo

Wananchi wa Kata ya Kitandililo, Wilaya ya Makambako Mjini, Mkoani Njombe wamemshukuru Rais Samia Suluhu kwa kuwajengea kituo cha Afya katika kata hiyo. 

Ujenzi huo utasaidia wakazi wa kijiji hicho hususasi kwa huduma za mama mjamzito pamoja na huduma zingine za dharura.

Wananchi hao iliwalazimu kutembea kilometa 35 kutoka katika kata hiyo hadi Makambako ambako wanaweza kupata huduma hizo umbali uliowalazimu kutumia gharama kubwa na kuhatarisha maisha yao kutokana na kuchelewa kupata huduma kutokana na umbali wa kukifata kituo cha afya.

Ikiwa ni mwaka mmoja wa Rais Samia Suluhu madarakani, takribani jumla ya shilingi bilioni  225 zimetengwa kutoka kwenye Trilion 1.3 za mpango wa ustawi na mapambano dhidi ya UVIKO-19 kwenda kwenye sekta ya afya.

Pamoja na ujenzi wa vituo vya afya pesa hizo pia zilitumika kuanzisha huduma za dharura “EMERGENCE MEDICAL DEPARTMENT” (EMD) katika Halmashauri 75, ujenzi wa majengo ya wagonjwa mahututi (ICU) 25 katika Halmashauri 25 , Ujenzi wa nyumba za watumishi wa afya pamoja na ununuzi wa vifaa na vifaa tiba.

 

error: Content is protected !!