Rais Samia anavyoifungua Kigoma kwa kuboresha Bandari ya Kibirizi

HomeKitaifa

Rais Samia anavyoifungua Kigoma kwa kuboresha Bandari ya Kibirizi

Dhamira ya kuurudisha Mkoa wa Kigoma kuwa kitovu cha biashara inaendelea kufanikishwa na Rais Samia Suluhu Hassan baada ya kuweka jiwe la Msingi la Upanuzi wa Bandari ndogo ya Kibirizi Kigoma ambayo ujenzi wake umefikia asilimia 69.5.

Mradi huo ni sehemu ya Mradi mkubwa unaohusisha Bandari za Tatu ambazo ni Kibirizi, Ujiji na Bandari kuu ya Kigoma ikijumuisha Ujenzi wa Gati, Majengo ya kupokea Mizigo, Jengo la abiria na Ofisi ambapo unagharimu Bilioni 32.

Uboreshwaji wa bandari hiyo ni moja wapo ya mikakati ya mapinduzi ya kiuchumi ya kuufanya Mkoa wa Kigoma kuwa kitovu cha biashara.

Aidha, katika uzinduzi huo Rais Samia Suluhu ametoa maelekezo kwa Wizara ya Ujenzi kuratibu Ujenzi wa Barabara ya kisasa ya kuingia kwenye Bandari hiyo huku akiita Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kuondoa vibanda vilivyojengwa nje ya Bandari na kutoa mchoro wa Ujenzi wa Soko la Kisasa.

 

error: Content is protected !!