Rais Samia aridhia miaka 30 kulipa Magomeni Kota

HomeKitaifa

Rais Samia aridhia miaka 30 kulipa Magomeni Kota

Wakala wa Mjengo Tanzania (TBA) umesema Rais Samia Suluhu ameridhia wakazi 644 wa Magomeni Kota, Dar es Salaam waongezewe muda wa ununuzi wa nyumba zilizojengwa na wakala huyo kutoka mika 15 hadi 30.

Awali, wakazi hao walitakiwa kununua nyumba hizo kwa miaka 15 na walipewa miaka mitano ya kuishi bure katika makazi hayo.

Mtendaji Mkuu wa TBA , Daud Kondoro alisema Dar es Salaam jana kuwa baada ya Rais Samia kuzindua nyumba hizo Machi 23 mwaka jana alitoa maelekezo ziuzwe kwa wakazi hao kama wakazi wanunuzi bila kuzingatia gharama za thamani ya ardhi, maeneo jumuishi kama ngazi, lifti na mandhari ya nje.

Gharama za nyumba hizo kwa chumba kimoja ni Shilingi milioni 48 na nyumba ya vyumba viwili inauzwa shilingi milioni 56.8 huku muda wa malipo ukiwa ni miaka 30 na miaka mitano ya kukaa bure.

error: Content is protected !!