Rais Samia: Hakuna atakayekosa shule

HomeKitaifa

Rais Samia: Hakuna atakayekosa shule

Wakati shule za msingi na sekdnoari nchini zikitarajiwa kufunguliwa Jamatatu ijayo, Rais Samia Suluhu amesema hakuna mwanafunzi atakayekosa nafasi ya kwenda shule kwa sababu ya uhaba wa madarasa.

Sambamna na hilo, Rais Samia amesema wiki ijayo serikali itaanza kuyatumia madarasa 8,000 yaliyojengwa katika kipindi cha siku 100 zilizopita ikiwa ni pamoja na samani zake nchi nzima, akiongeza kuwa hatua hiyo ni ukombozi kwa wanafunzi zaidi ya 400,000.

Rais Samia aliyasema hayo kupitia ujumbe wake aliouweka jana katika akaunti yake ya Twitter ambapo alisema kutokana na mafanikio hayo hakuna mwanafunzi atakayekosa nafasi ya kwenda shule kwa sababu ya uhaba wa madarasa.

error: Content is protected !!