Rais Samia: Serikali itaendelea kutoa ruzuku kushusha bei ya mafuta

HomeKimataifa

Rais Samia: Serikali itaendelea kutoa ruzuku kushusha bei ya mafuta

Hakuna mama anayependa kuona mtoto wake anateseka wala kupitia changamoto, lazima atafanya juhudi ili aweze kumsaidia kwa namna moja au nyingine. Hili limethibitika nchini kwetu ambapo tunaona namna ambavyo Rais Samia Suluhu anavyojitahidi kuhakikisha anapunguza makali tunayopata kwenye mfumuko wa bei ya mafuta.

Wakati dunia ikikumbwa na shida ya upatikanaji wa mafuta ya petroli, dizeli na mafuta ya taa hadha iliyosababishwa na vita katika ya Urusi na Ukraine, serikali ya awamu ya sita ikiongozwa na Rais Samia inatoa ruzuku ya Sh bilioni 100 kila mwezi kwa ajili ya kukabiliana na na ukali wa bei ya mafuta mpaka hapo hali itakaporejea kuwa kawaida.

“Tutaendelea kutoa hiyo ruzuku mpaka duniani kukae sawa. Tutaendelea kukata shilingi bilioni 100 kila mwezi kwenye matumizi ya serikali ili tuweke ruzuku kwenye mafuta mpaka bei zikae sawa , hiyo ni kupunguza makali ya mafuta, kwa hiyo zitakuwa zinashuka mpaka tufikie bei zilivyokuwa,” alisema Rais Samia.

Maana ya bilioni 100 kwa wananchi

Upendo na kujali maslahi ya wananchi

Kutolewa kwa shilingi bilioni 100 ni dhahiri kwamba Rais Samia anathamini wananchi wake na ndio maana akaamua kuinyima serikali ili tupate ahueni.

Waziri wa Nishati, January Makamba aliweka wazi hili kwamba bei ya mafuta haijashuka bali imeshushwa na Rais Samia Suluhu.

“Rais Samia ameyashusha (mafuta) na asingeyashusha yangekuwa zaidi ya shilingi 3,700, kwa kuwa kule yanakotoka bei inaendelea kupanda,” – Waziri wa Nishati, January Makamba.

Kupunguza ukali wa maisha

Bilioni 100 inayotolewa itaenda kupunguza ukali wa maisha kwani kama isingetolewa wananchi wangekuwa wanatumia fedha nyingi kwenye ununuzi wa mafuta.

Ikumbukwe hivi sasa lita moja ya mafuta ya petroli inauzwa Sh 2,994 kwa Mkoa wa Dar es Salaam, 2,985 kwa Mkoa wa Tanga na 2,979 kwa Mkoa wa Mtwara, kwa upande wa dizeli imeshuka kutoka Sh 3,452 hadi 3,131 kwa Dar es Salaam, 3,162 kutoka 3,693 kwa Mkoa wa Tanga na Sh 3,165 kutoka 3,650 kwa Mkoa wa Mtwara.

Hatua hii iliyochukuliwa na Serikali ya Awamu ya sita itaenda kupunguza gharama za maisha kwa Watanzania, amabo siku za hivi karibuni, walishuhudia bei za bidhaa na huduma mbalimbali zikipaa.

error: Content is protected !!