Rais Samia: Wanafunzi wapewe ujuzi mpya

HomeKitaifa

Rais Samia: Wanafunzi wapewe ujuzi mpya

Rais Samia amewaagiza mawaziri wanaosimamia Wizara ya Habari na Teknolojia ya Mawasiliano na ile ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kuweka mipango ya kuwapatia ujuzi mpya wanafunzi wa shule za msingi hadi vyuo vikuu unaoendana na kasi ya mabadiliko ya teknolojia duniani.

Kiongozi mkuu huyo wa nchi amesema kwa sasa dunia inapita katika wimbi la nne la mapinduzi ya viwanda ambao unahusisha zaidi matumizi ya teknolojia za kisasa katika utendaji na uzalishaji. 

Amesema, kutokana na hali hiyo, wanafunzi wa Tanzania wanatakiwa kupata ujuzi unaendana na mabadiliko hayo ili wasiachwe nyuma. 

“Napenda kuzikumbusha wizara za Mawasiliano na Teknolojia, Wizara ya Elimu na vyuo vikuu vyote kuwa tupo katika wimbi la nne la mapinduzi ya viwanda.

“Wanafunzi kuanzia shule za msingi hadi vyuo vikuu wanahitaji ujuzi mpya. Ujuzi ambao ni tofauti na ule wa wahitimu wa miaka iliyopita kama alivyosema Jaji Mkuu (Profesa Ibrahim Juma) hapa,” amesema Rais Samia.

Rais Samia aliyekuwa akizungumza katika kilele cha Wiki ya Sheria nchini Tanzania leo Februari 2, 2022 jijini Dodoma amesema wanafunzi wanatakiwa kutayarishwa kufanya kazi zinazohitaji ujuzi unaolingana na matakwa ya mabadiliko ya teknolojia.

error: Content is protected !!