Sababu 7 za kwanini bado upo ‘single’

HomeElimu

Sababu 7 za kwanini bado upo ‘single’

Je, unadhani unazeeka na hakuna anayekuvutia? Una wasiwasi hakuna mtu anataka kukuchumbia? : Sio kweli kwani kila jambo na wakati wake, huenda huu sio muda muafaka wa wewe kuwe kwenye mahusiano.Pia, kuwa ‘single’ sio dhambi wala makosa, na inaweza kusababishwa na sababu nyingi tu zinazoweza kuwa ndani au nje ya uwezo wako.

Kuna sababu zinazopelekea mtu kuwa ‘single’ nazo ni;

1. Mahusiano yaliyopita
Achana na yaliyopita na karibisha mpya. Matukio yenye kuumiza na mabaya kutoka kwa mahusiano ya awali yanaweza kukuvuruga kihisia lakini ukiyazingatia, hutawahi kuendelea. Inaweza kuwa ngumu lakini jaribu kujiponya na kujisamehe mwenyewe na/au ‘ex’ wako. Msamaha huweka akili yako huru na kukufungua kwa matukio mapya.

2. Kukutana na watu ambao sio sahihi
Wakati mwingine ni bahati mbaya tu. Kuna uwezekano mkubwa umekuwa ukikutana na watu wasiofaa na hii inaweza kuvuruga akili yako. Watu wasio sahihi wangekuacha ukijiuliza shida yako ni nini. Lakini usijali kuhusu hilo. Uko sawa kabisa, mtu sahihi yuko karibu na utakutana naye hivi karibuni.

Faida 5 za kuwa ‘Single’

3. Hofu ya kujitoa (kufanya jitihada)
Baadhi yetu tunaogopa sana kujitoa, na hii ni kwa sababu tumepoteza juhudi zetu katika mahusiano ya zamani. Ikiwa hili ni tatizo lako, jua kwamba hauko peke yako, wengi tunaogopa. Lakini, ikiwa unataka kuishi maisha ya ndoto zako, unahitaji kushinda hofu hii. Jaribu uhusiano mpya, usiweke shinikizo nyingi kwa mpenzi wako ujao.

4. Maisha ya jamii
Je, wewe ni msumbufu katika jamii? Je, unapenda kuwa ndani ya nyumba? Je, wewe ni mchapa kazi kamili? Hii inaweza kuwa sababu ya hali yako ya pekee. Legeza kidogo, maisha ni mafupi. Tumia wakati na marafiki zako, cheza nao. Huwezi kujua ni nani unaweza kukutana naye.

5. Kupenda kuchagua sana
Hakuna mwanadamu mkamilifu wala hakuna uhusiano mkamilifu. Chagua kuwa na mtu ambaye ana viwango unavyotamani na jifunze kuvumilia/kupuuza dosari zao zisizo na maana. Acha kusumbua pia, haisaidii mtu yeyote. Mfano mtu kuchagua kuhusu maumbile au hali ya maisha ya mwenzake.

6. Mtazamo wako
Je, kila mtu anasema wewe ni mkorofi? Labda, wanaweza kuwa sawa kidogo. Jaribu kuwa na adabu kwa watu/wageni. Unaweza kuwa mtu wakifahari na bado kuwa na utu kubwa. Njia moja ni kutabasamu mara nyingi, inasaidia sana.

Mjue mtu sahihi kuanzisha naye mahusiano

7. Kiwango chako cha usafi
Hili ni mojawapo ya matatizo ambayo hayazingatiwi. Kiwango chako cha usafi ni muhimu sana. Ikiwa huna harufu nzuri, usipovaa vizuri, ukiwa na harufu ya mdomo au harufu ya mwili, basi jua kabisa hakuna mtu atakayehamia kwako.

Kwa hiyo kabla ya kumlaumu shetani, angalia usafi wako.

error: Content is protected !!