Sabaya alivyoachiwa huru na Mahakama kwa kujifanya Afisa usalama

HomeKitaifa

Sabaya alivyoachiwa huru na Mahakama kwa kujifanya Afisa usalama

Sabaya alivyoachiwa huru na Mahakama kwa kujifanya Afisa usalama

Agosti 2016 Polisi mkoani Arusha walimkamata aliyekuwa Diwani wa Kata ya Sambasha (CCM) iliyopo Wilayani Arusha vijijini, Lengai Ole Sabaya kwa kosa la kujifanya Afisa Usalama wa Taifa.

Sabaya ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Mkoa wa Arusha wakati huo mbali na kujifanya Afisa Usalama wa Taifa alishtakiwa kwa kughushi kitambulisho cha idara hiyo.

    > Sabaya alivyowataja Magufuli na Mpango mahakamani kwenye

Katika kesi hiyo alidaiwa kuwa Mei 18 mwaka 2016 katika Hotel ya Sky Motel alijifanya Afisa usalama wa Taifa na kupata huduma ya kulala katika hotel hiyo na kupata chakula na vinywaji wakati siyo kweli.

Aidha, alishtakiwa kwa kosa la pili la kughushi kitambulisho kilichosomeka MT.86117 wakati akijua wazi kuwa kufanya hivyo ni kosa kisheria.

Baadaye Sabaya aliachiwa huru baada ya upande wa Jamhuri kushindwa kuthibitisha tuhuma zilizokuwa zinamkabili Sabaya.

error: Content is protected !!