Samia atoa milioni 500 kwa ajili ya  maji

HomeKitaifa

Samia atoa milioni 500 kwa ajili ya maji

Rais Samia Suluhu anazidi kuzinufaisha mamlaka za maji baada ya kuagiza zipatiwe Sh milioni 500 kama mkopo kwa ajili ya kusaidia uunganishaji maji kwa wananchi kwa haraka.

Akizindua mradi wa maji wa Kyala- Bunazi wilayani Missenyi, mkoani Kagera jana, aliagiza Wizara ya Maji kuta kiasi hicho cha fedha kwa mamlaka za mkoani Kagera zisimamiwe ili zikisharejeshwa, zitumike pia katika mamlaka nyingine za maji.

“Sasa katika mambo haya mazuri wananchi watakuwa na hamu ya kuunga maji kwa sababu yanapatikana, akina mama watataka bomba la maji liwe nyumbani. Sasa ili twende na msemo wa kazi iendelee, Naomba muwakopeshe mamlaka za maji za maeneo haya shilingi milioni 500, iwe ni nyenzo ya kuunga maji kwa wananchi kwa haraka haraka,” aliagiza Rais Samia.

Alisema ana uhakika fedha hizo zikitumika kuwaunganishia wananchi mahi na kusimamiwa vyema katika marejesho yake, zitatumika pia katika mamlaka nyingine za maji na kuendelea kuwuanganishia maji wananchi kwa haraka.

Kuhusu gharama za maji, Rais Samia alisema, serikali imefanya kazi nzuri kupekela maji vijijini na mijini ingawa haijamaliza kazi hiyo.

error: Content is protected !!