Sangara wapungua Ziwa Victoria

HomeKitaifa

Sangara wapungua Ziwa Victoria

Samaki aina ya sangara wamepungua katika Ziwa Victoria kutoka tani 537,479 mwaka 2020 hadi tani 335,170 kwa mwaka 2021.

Ofisa Uvuvi wa Mkoa wa Mwanza, Titus Kilo alisema hayo alipokuwa akiwasilisha taarifa ya maendeleo ya sekta ya uvuvi na mikakati ya kuboresha sekta hiyo kwenye kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Mwanza.

Alisema kupungua kwa samaki hao kumegundulika kutokana na tathimini ya kubaini wingi wa samaki ziwani iliyofanyika kati ya mwaka 2020 na 2021.

Alisema kushuka kwa idadi ya sangara katika Ziwa Victoria kumetokana na sababu mbalimbali ikiwemo kuongezeka kwa shughuli za uvuvi na uvuvi haramu.

Alisema sangara wengi walioko ziwani kwa sasa ni sangara wadogo wenye urefu wa chini ya sentimeta 50. Hata hivyo alisema dagaa wameongezeka kutoka tani 430,359 mwaka 2020 hadi tani 557,479 mwaka 2021.

error: Content is protected !!