Serikali imelipa jumla ya Sh bilioni 954.04 ikiwa ni madai ya VAT sawa na asilimia 431.7 ya lengo la kulipa Sh bilioni 221.01 kwa mwaka 2021/22, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Hamad Hassan Chande ameliambia Bunge mjini Dodoma.
Akijibu swali la mbunge wa Njobe Mjini Deodatus Manyika, Chande amesema ufanisi huo umetokana na hatua zilizochukuliwa na serikali kuhakiki maombi ya wadai kwa kizingatia viashiria hatarishi badala ya utaratibu wa awali wa kuhakiki maombi yote kwa asilimia 100.
Mwanyika alikuwa amehoji ni kiasi gani kimerudishwa kwa wadai wa VAT wanaodai Serikali.
“Utaratibu huo umeongeza kasi ya uhakiki na ulipaji wa madai ya marejesho ya VAT na kupunguza ucheleweshwaji kwa kuwa uhakiki unafanyika kwa wakati. Hatua na mafanikio hayo yanalenga kuchochea ukuaji wa uchumi, uwekezaji na kulinda mitaji ya wawekezaji na wafanyabiashara hapa nchini.