Serikali kufikisha umeme vijiji vyote 2030

HomeKitaifa

Serikali kufikisha umeme vijiji vyote 2030

Serikali ya Tanzania imedhamiria kuimaliza changamoto ya ukosefu wa umeme katika vijiji vyote vya nchi hiyo ifikapo mwaka 2030.

Serrikali imeonyesha mwenendo wa kuridhishwa na mradi wa umeme vijijini chini ya wakala wa umeme (REA) tangu kuanza kwa miradi huo mwaka 2007 na kukiri kwamba REA wamepiga hatua ya kuridhisha.

Kwa upande wake, Mkurugenzi mkuu wa REA, Mhandisi Hassan Saidy, amesema kua; “Wakati REA inaanzishwa mwaka 2007, upatikanaji wa umeme vijijini ulikuwa ni wa aslimia mbili tu (2%), lakini mpaka sasa ufikiwaji huo wa umeme vijijini umefikia asilimia sitini na tisa na pointi sita (69.6) na ifikapo mwaka 2030, umeme utapatikana kwa asilimia mia (100%) ikiwa na maana ya umeme kufika katika vijiji vyote vya Tanzania.

Changamoto ya umeme imekua ni suala ambalo linashughulikiwa kwa kasi kubwa na serikali ya Tanzania. Kwa ajili ya kuhakikisha upatikanaji wake katika maeneo yote ya Tanzania pamoja na uvunaji wa umeme wa uhakika utakaorahisisha shughuli za kimaendeleo nchini humo.

error: Content is protected !!