Serikali kujenga shule za wasichana 26, na za kata 1,000

HomeKitaifa

Serikali kujenga shule za wasichana 26, na za kata 1,000

Serikali imepanga kuanza kutekeleza mpango wa ujenzi wa shule za sekondari za wasichana kila mkoa na nyingine 1,000 kwenye kata zisizokuwa na sekondari ili kupunguza msongamano madarasani na kuondoa adha za kutembea umbali mrefu hususan kwa wasichana.

Kwa mujibu wa Naibu wa Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Deo Silinde, Serikali imetenga shilingi bilioni 220 kwa ajili ya utekelezaji wa awamu ya kwanza ya mpango huo itakayoanza mwaka wa fedha 2021/22.

Silinde ameeleza kwamba mpango huo pia unahusisha upanuzi wa shule za sekondari 100 ili ziweze kupokea wanafunzi zaidi wa kidato cha tano na sita.

error: Content is protected !!