Sh. bilioni 80 kuendeleza Bandari ya Mbamba Bay

HomeKitaifa

Sh. bilioni 80 kuendeleza Bandari ya Mbamba Bay

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania- TPA imeingia Mkataba wa usanifu na ujenzi wa uendelezaji wa Bandari ya Mbamba Bay iliyopo wilayani Nyasa Mkoani Ruvuma.

Waziri wa Uchukuzi Mhe. Prof. Makame Mnyaa Mbarawa ameshuhudia utiaji saini wa mkataba huo, utakaogharimu shilingi Bilioni 80 na unaotarajia kukamilika katika kipindi cha miezi 24.

Akizungumza katika hafla ya utiaji saini mkataba huo tarehe 4 Desemba, 2023, Mhe. Prof. Mbarawa amesema ujenzi wa Bandari hiyo itakayokuwa Makao makuu ya Bandari za Ziwa Nyasa, unafanywa na kampuni ya Xiamen Ongoing Construction Group Co. Ltd ya China, utakapokamilika utaongeza ufanisi wa Bandari ya Dar es Salaam na ushoroba wa Mtwara na hivyo kuongeza fursa za ajira na kuinua uchumi.

error: Content is protected !!