Msanii wa BongoFleva Shilole ametambulisha rasmi wimbo wake mpya wa Mama Ntilie unaendelea kufanya vizuri katika mitandao mbalimbali tangu siku ya kuachiwa kwake.
Wakati akifanya utambulisho wa wimbo huo kwenye vituo vya habari mbalimbali, Shilole aliweka wazi kwamba wimbo umeandikwa na Barnaba na kwamba yeye hausiki na mashahiri yaliyomo ndani ya ngoma hiyo.
“Nimekuta ameandika akaniambia Shishi njoo kuna nyimbo nataka uimbe basi, kwahiyo idea ni yakwake mimi nimeimba tu. Na kaniambia wakileta tena masihara anangoma nyingine,” alisema Shilole.
Alivyoulizwa kuhusu maneno ya aliyewahi kuwa mpenzi wake miaka ya nyuma Nuh Mziwamba, Shilole akasema hapendezwi na tabia ya Nuh na kwamba ipo siku atampiga makofi kama ataendelea na tabia yake.
“Mimi ni mkali kweli kweli sio masihara, kama unaingia kwenye anga zangu yule mtoto kuna siku nitakuja kumkatama nimtie makofi namsubiri,” alisema Shilole.
Ameongea hayo alipokuwa akihojiwa kwenye redio ya East Africa na kuongeza kuwa sasa amerudi rasmi kwenye muziki baada ya kukaa kimya kwa muda huku akitoa sababu ya kuwa alikua anasimamisha biashara yake ya Shishi Food.