Sifa 5 za kocha ambaye Simba inamuhitaji

HomeMichezo

Sifa 5 za kocha ambaye Simba inamuhitaji

Mabingwa wa soka Tanzania Simba, wanatarajia kumtangaza kocha wao mpya siku yoyote kuanzia Jumatatu Novemba 8,2021.

Baada ya kuachana na Mfaransa Didier Gomes Da Rosa, Simba inahitaji kocha mwenye sifa zitakazoisidia timu hiyo kurejesha makali ambayo yameonekana kupungua katika mechi za mwanzoni mwa msimu huu.

Sifuatazo ni sifa za lazima kwa kocha huyo;

5. Leseni ya ‘UEFA A Pro’ au ‘CAF A’ 

Moja kati ya sababu zilizofanya Simba ikose huduma ya kocha Gomes Da Rosa aliyewapa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu uliopita ni kocha huyo kukosa Leseni daraja a ya Shirikisho la Mpira Afrika (CAF) au Leseni ya ‘UEFA A Pro’.

Bila shaka hiii itakuwa sifa ya kwanza kwa kocha atakayetambulishwa na Simba wiki ijayo, lazima awe na leseni zinazotakiwa.

4. Uzoefu

Simba haiko katika majaribio, inahitaji matokeo na hivyo lazima kocha atakayetambulishwa na ‘Wekundu wa Msimbazi’ awe na uzoefu wa kutosha katika kazi hiyo.

3. Kufahamu soka la Afrika

Kati ya mambo yanayowapa hasira wapenzi na wanachama wa Simba kwa sasa ni kitendo cha timu yao kutolewa mapema kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka huu.

Simba wanataka kutetea sifa yao katika soka la Afrika, hivyo kocha anayehitajika ndani ya timu hiyo lazima awe  na ufahamu wa kutosha kuhusu soka la Afrika.

2. Uwezo wa kuunganisha timu (Umoja)

Kabla ya kuondoka kwa Didier Gomes Da Rosa zilizuka tetesi kwamba  ndani ya Simba kuna mpasuko mkubwa. Tetesi zilidai kwamba kocha Gomes amewagawa wachezaji.

Kocha atakayetambulishwa na Simba lazima awe na uwezo wa kuwaunganisha wachezaji pamoja na benchi lote la ufundi.

Kama ilivyo kauli mbiu ya Simba, ‘Nguvu Moja’, umoja ni nguzo muhimu sana katika kuipatia Simba matokeo.

1. Uwezo wa kuhimili shinikizo kutoka nje ya uwanja.

Kocha huyo atakutana na Simba ambayo ina shinikizo kubwa kutoka kwa mashabiki ambao hawafurahishwi na matokeo ya timu yao kwa sasa, shinikizo kutokana na kiwango cha waatani wao wa jadi Yanga ambao wanaonekana kuwa na nguvu mpya na shinikizo kutoka kwa uongozi ambao umepitia mabadiliko hivi karibuni baada ya kujiuzulu kwa Mohammed Dewji aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya timu hiyo.

Kocha mpya wa Simba, lazima awe mtulivu na mvumilivu

error: Content is protected !!