Kamati iliyoundwa kuchunguza kupanda kwa bei ya mafuta (petroli, dizeli na mafuta ya taa) imewasilisha ripoti yake kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
Hayo yamesemwa leo Oktoba 02, 2021 na Msemaji na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa alipokuwa na mkutano na waandishi wa habari mkoani Morogoro katika muendelezo wa utoaji ripoti za utendaji wa Serikali anayoitoa kila wiki.
“Serikali kupitia kwa Waziri Mkuu [Kassim Majaliwa] ilisitisha bei mpya zilizotangazwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) mpaka zitathiminiwe kwanza yale maeneo yote yanayotengeza bei ya bidhaa ya mafuta.
> Saba wafariki ajalini Dodoma
Kamati ile iliyokuwa imeundwa na Waziri Mkuu imeshakamilisha kazi yake imekabidhi ripoti juzi na Waziri Mkuu ameikabidhi kwa Waziri wa Nishati [January Makamba] na yeye anaifanyia kazi na wakati wowote Serikali itakuja kuwaambia uamuzi wake juu ya eneo hili,” amesema Msigwa.
Kamati hiyo iliundwa Septemba 02, 2021 na ilipewa wiki mbili kukamilisha kazi ya kuchunguza kupanda kwa bei ya mafuta.