HomeKitaifa

Tahadhari kirusi kipya cha Corona

Wizara ya Afya Tanzania imetoa tahadhari kwa Watanzania kuendelea kufuata ushauri wa wataalamu wa afya kujikinga na maambukizi ya kirusi kipya cha Corona baada ya Shirika la Afya Duniani (WHO), kuripoti uwepo wa aina mpya ya kirusi cha Uviko-19 kiitwacho “Omicron”, kinachosemekana kuwa na uwezo wa kusambaa haraka.

Mambo yakuzingatia ili usipate kirusi hicho ni pamoja na kuhakikisha umepata chanjo ya Uviko-19, zingatia uvaaji barakoa na kunawa mikono kwa sabuni na maji tiririka, fanya mazoezi na kutumia tiba asili kutokana na maelekezo ya wataalamu pamoja na kuepuka mikusanyiko na safari zisizozalazima.

Pia Wizara ya Afya imewataka wananchi kuendelea na shughuli za uzalishaji huku wakichukua tahadhari dhidi ya kirusi hicho kipya.

error: Content is protected !!