Tahadhari kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT)

HomeKitaifa

Tahadhari kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT)

Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imewataka Watanzania kuwa makini na utapeli mpya unaofanyika kwa njia ya barua pepe unaoelekeza kulipa kiasi fulani cha fedha kuwezesha kupata fedha nyingi.

BOT katika taarifa yake iliyotolewa leo Januari 6, 2022  imebaini kuongezeka kwa udanganyifu wa fedha nchini unaohusisha mwananchi kupokea taarifa (hati au barua pepe) inayodai kuwa ni uthibitisho wa malipo kupitia SWIFT na/au mifumo mingine ya uhamishaji fedha.

“Mpokeaji anafahamishwa kuwa fedha zimeingizwa kwenye benki au akaunti katika taasisi ya fedha nchini Tanzania; wakati mwingine, mpokeaji fedha anaelekezwa kulipa kiasi fulani cha fedha kuwezesha kupata fedha hizo nyingi,” imeeleza taarifa ya BoT

Matukio mengi ya taarifa hizo yanahusisha kiasi kikubwa cha pesa kinachodaiwa kuletwa kwa ajili ya ufadhili wa mradi au matumizi binafsi.

Benki Kuu imesema taarifa hizo ni za kughushi na za kubuni na kusema “wananchi mnashauriwa kuwa waangalifu na kuacha kujihusisha na miamala hiyo ambayo kwa kawaida inalenga kuwatapeli fedha.”

error: Content is protected !!