Tanapa yapiga marufuku uvaaji wa sare zake

HomeKitaifa

Tanapa yapiga marufuku uvaaji wa sare zake

Jeshi la Uhifadhi wa Wanyamapori na Misitu la Mamlaka ya Hifadhi ya Taifa (TANAPA) imeagiza watu waache kuvaa sare zake popote.

Taarifa hii imetolewa na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi- Mawasiliano na Habari wa Tanapa, Pascal Shelutete, ilisema hivi karibuni kumekuwa na matukio holela ya uvaaji wa sare hizo katika jamii.

“Hali hiyo imetokea pengine kwa kutojua hivyo ni kinyume na sheria iliyounda Jeshi la Uhifadhi wa Wanyamapori na Misitu Na 5 ya mwaka 2009 pamoja na marekebisho yake kupitia sheria ya marekebisho Na 2 ya mwaka 2020,” ilieleza taarfia hiyo.

Shelutete alieleza kuwa jeshi hilo halitasita kuchukua hatua za kisheria kwa watakaobainika kukiuka tahadhari hiyo.

error: Content is protected !!