Tanzania kuandaa mkutano wa UNESCO

HomeKitaifa

Tanzania kuandaa mkutano wa UNESCO

Tanzania imepewa nafasi ya kuandaa mkutano mkubwa wa maadhimisho ya miaka hamsini (50) ya utekelezaji wa mkataba wa 82 wa UNESCO utakaofanyika leo tarehe 12-14 desemba mwaka huu wa 2022.

Mkutano huo unaolenga kuwezesha uelewa wa pamoja kuhusu utambuzi wa uhifadhi wa mali asili za dunia na namna ya kuandaa wataalamu hasa kwa vijana kwa kuzingatia jinsia, umepangwa kufanyika huko Jijini Arusha Tanzania.

Kwa mujibu wizara ya maliasili na utalii, Mkutano huu ni matunda ya filamu ya Tanzania Royal Toor, filamu iliyoipambanua vyema Tanzania katika uso wa dunia juu ya masuala mazima ya mali za asili pamoja na utalii.

“Tunatarajia mara baada ya mkutano huu wageni wetu watapata fursa ya kutembelea vituo vya utalii ili kuwa mbalizi watakaporudi kwenye nchi zao.” amesema Waziri wa maliasili na utalii Dr. Pindi Chana.

Mkutano huo unatarajiwa kuhudhuriwa na wageni wasiopungua mia moja (100) kutoka mataifa mbalimbali duniani.

error: Content is protected !!