TANZIA: Kiroboto afariki dunia

HomeKitaifa

TANZIA: Kiroboto afariki dunia

Mpiga matarumbeta maarufu King Kiroboto OG amefariki dunia usiku wa kuamkia leo baada ya kudondoka akiwa kwenye shoo katika Hoteli ya Giraffe, Temeke jijini Dar es Salaam.

Taarifa kutoka kwa watu wa karibu wa msanii huyo, zinaeleza kwamba alikuwa kwenye shoo ambapo baadaye alielekea maliwatoni lakini hakurudi, baadaye akakutwa akiwa ameanguka chooni.

Taarifa zinazidi kueleza kuwa, alikimbizwa Hospitali ya Temeke lakini ikabainika kwamba tayari amefariki dunia ambapo taratibu za mazishi zinafanyika nyumbani kwao kijichi Jijini Dar es Salaam.

error: Content is protected !!