Tetesi za Soka Ulaya leo Oktoba 13 (Chamberlain mbioni kurudi Arsenal, Man City ikimnyatia Haaland)

HomeMichezo

Tetesi za Soka Ulaya leo Oktoba 13 (Chamberlain mbioni kurudi Arsenal, Man City ikimnyatia Haaland)

Klabu ya Liverpool ipo tayari kumuuza kiungo wake Oxlade-Chamberlain (28), kwa bei stahiki huku kukiwa na taarifa zinazomhusisha kurudi Arsenal (Mirror).

Liverpool pia imeanza mazangumzo na Barcelona juu kumsajili mshambuliaji wake Ousmane Dembele (24) mchezaji huyo atakapo maliza mkataba wake msimu ujao (Mundo Deportivo).

Mshambuliaji wa Manchester City Raheem Sterling (26), anataka kuhakikishiwa kwamba ni sehemu muhimu ya mipango ya kocha Pep Guardiola kabla ya kuanza tena mazungumzo ya mkataba na Manchester City (Sun).

Kiungo wa kati wa England Phil Foden 21, yupo katika hatua za mwisho kutia saini mkataba mpya Manchester City. Ambapo mkataba wake wa sasa unamalizika mwaka 2024 (The Athletic).

> Tetesi za Soka Ulaya leo Oktoba 12 (Lacazette mbioni kuachana na Arsenal, huku safari ya Hazard kurudi Chelsea imepamba moto)

Klabu ya Manchester United imeungana na Chelsea na Juventus katika mbio za kumsaka kiungo wakati wa Monaco na Aurelien Tchouameni, 21 (Express).

Wakala wa Erling Haaland, Mino Raiola anatarajiwa kufanya mazungumzo na Manchester City kuhusu uwezekano wa usajili wa mshambuliaji huyo wa Borussia Dortmund majira ya kiangazi (Times).

Mchezaji wa Arsenal Hector Bellerin (26) amedokeza kwamba hana nia ya kurejea tena Arsenal mkataba wake wa mkopo Real Betis utakapokwisha (El Desmarque).

Beki wa Barcelona Clement Lenglet 26, huenda akawa wa mchezaji kwanza kusajiliwa na klabu ya Newcastle baada ya klabu hiyo kununuliwa hivi karibuni. Inasemekana mchezaji huyo anahitajika klabuni hapo (Sport.es).

Beki wa Ujerumani Antonio Rudiger, 28, anatathmini hali ilivyo kabla ya kufanya uamuzi juu ya mustakabali wake katika klabu ya Chelsea, huku mkataba wake wa sasa ukitarajiwa kumalizika mwisho wa msimu (Sky Sports).

Southampton,Tottenham na West Ham wapo kwenye kinyang’anyiro cha kupata saini ya kipa wa West Brom  Sam Johnstone, 28 (Hampshire Live).

Klabu ya Leeds United wapo hatua za mwisho kumsajili mshambuliaji wa Espanyol ya Hispania Mateo Joseph Fernandez (17). Leeds wamewasilisha dau la pauni £450,000, lakini Espanyol wanatakapauni milioni moja (Team Talk).

error: Content is protected !!