Kiungo wa kati wa Marseille Dimitri Payet 34, anasema anashangazwa sana kuona beki, William Saliba (20) hapewi nafasi ya kucheza klabuni hapo kama ilivyokuwa katika klabu yake ya Arsenal (L’Equipe via Metro). Saliba anakabiliwa na wakati mgumu haswa katika kuonyesha uwezo wake, hii ni changamoto iliwahi kumkuta Romelu Lukaku lakini hakukata tamaa akapambana na kufanikiwa kuonyesha ubora wake.
Manchester City ina mpango kuziba nafasi ya mshambuliaji Raheem Sterling 26, na mshambuliaji wa Bayern Munich, Robert Lewandowski, 33 (Express). Nidhamu na kujituma ni moja ya sifa zinazohitajika katika michezo, mgogoro uliopo baina ya Sterling na kocha wake Pep Guardiola ndio unapelekea kuzaliwa kwa yote haya kutokana na utukutu wa Sterling.
Mshambuliaji wa Paris St-Germain Kylian Mbappe 22, hatasaini mkataba mpya na bila kujali mshahara atakaolipwa na timu hiyo ya Ligue 1 kwani ameamua kujiunga na Real Madrid (AS – Spanish). Mbappe kwa sasa anaangalia mustakabali wa kuchezea timu yake aliyoilenga toka utotoni ili kutimiza malengo yake aliyojiwekea, jambo jema kila la kheri Mpappe.
> Tetesi za Soka Ulaya leo Oktoba 15 (Lingard kuachana na Man United mwezi January, huku Klabu ya Liverpool ikimnyatia Raphinha)
Klabu za Liverpool, Manchester City na Manchester United zote zipo katika mbio za kupata saini ya kiungo wa kati wa Monaco Aurelien Tchouameni 21, ambaye anakadiriwa kuwana thamani ya pauni milioni 40 (ESPN). Uhai wa timu iwapo uwanjani nikuwa na kiungo anayeweza kuichezesha timu ambapo sifa hizi zinapatikana kutoka kwa Tchouameni.
Kocha wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer anakubali kwamba kiungo Jesse Lingard (28) huenda asishawishike kusaini mkataba mpya klabuni hapo isipokuwa apate muda zaidi wa mchezo (Evening Standard). Hatua anazozichukua Lingard ni sahihi kabisa katika Maisha yake ya soka kwa maana ili yeye azidi kung’ara katika soka ni lazima acheze kuonyesha kipaji chake.
Wakala wa Paul Pogba (28) Mino Raiola amempa ofa kiungo huyo wa Manchester United kwa Barcelona. Mkataba wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa na Manchester United unatarajiwa kumalizika mwisho wa msimu ujao, Raiola pia amewasiliana na Juventus, Paris St-Germain, Real Madrid na vilabu kadhaa vya Ligi Kuu (ESPN). Poga ni mchezaji muhimu ndani ya united na kuondoka kwake kutaiteteresha timu uwanjani mpaka pale atakapopatikana mchezaji wa kuziba nafasi yake United wanapaswa kutambua hili na kulifanyia kazi.
Mshambuliaji wa Everton Dominic Calvert-Lewin 24, atakuwa lengo kuu la Arsenal msimu ujao wa usajili (Sports London). Klabu ya Arsenal imekuwa ikisuasua katika kiwango chake cha uchezaji uwanjani na pale wanapocheza vizuri safu ya umaliziaji huwa tatizo ambapo suluhisho lake ni kuwa na mshambuliaji mwenye njaa ya kufunga magoli.
Kocha wa Roma, Jose Mourinho ana nia ya kumsajili kiungo wa Barcelona, Riqui Puig 22, ambaye kiwango chake kimeshuka chini ndani ya Nou Camp (Sport in Spanish). Hii ni moja ya nafasi nzuri kwa Puig kwenda kujiimarisha na kuonyesha ubora wake.
Wawakilishi wa Declan Rice (22) wamepuuza taarifa zinazomhusisha kiungo wa West Ham 22, na kuhamia Newcastle (90Min). Kwa sasa klabu ya Newcastle inahusishwa na wachezaji wengi wenye vipaji na kujituma uwanjani ambao wanaweza kuja kuinua timu hiyo iendane na uwekezaji uliofanyika hivi karibuni, niwatakie kila kheri.