Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini ndugu Mussa Makame amefanya ziara yake Mkoani Mtwara na kutembelea kitalu cha Gesi asilia cha Mnazi Bay kijiji cha Msimbati Mtwara.
Akizungumza na waandishi wa habari Septemba 28’2023 Ndugu Makame amesema visima vyote vitano vya Gesi vinafanya kazi na vina gesi ya kutosha kwa matumizi ya shughuli za huduma za umeme, matumizi ya nyumbani mpaka kwenye magari.
“Uzalishaji wa visima vyote vitano hapa hapa (Kitalu cha Mnazi Bay) unaendelea , hakuna tatizo lolote wala hakuna ukweli wowote kwamba kuna kisima kimekauka au visima havitoi gesi sasa hivi,” amesema.
Katika hatua nyingine ndugu Makame amekanusha taarifa iliyosambaa mtandaoni inayosema visima vya Gesi asilia Mkoani Mtwara vimekauka huku akisema kuwa Bado Gesi ipo ya kutosha.