Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Ujerumani wameipata Tanzania msaada wa Shilingi bilioni 209,746,204,779.00 kwa ajili ya masuala mbalimbali ya kijamii na nchi kwa ujumla.
Kupitia ukurasa wake wa mtandano wa twitter, Waziri Nchemba alisema tayari majadiliano yameshakamilika na wameahidi kutumia fedha hizo kwenye maeneo yaliyokusudiwa.
Tumemaliza majadiliano na Ujerumani, wameipatia Tanzania Msaada wa TZS 209,746,204,779.00 kwa ajili ya kusaidia masuala ya sekta ya Afya, Maji, Uwezeshaji wa wanawake,Ulinzi wa bioanuwai,kuzuia rushwa, mfumo wa Kidijitali,kuunganisha kaya na maji ya kunywa na usafi wa Mazingira. pic.twitter.com/HDB05HwYKv
— Mwigulu Nchemba, PhD (@mwigulunchemba1) November 17, 2022