Uongozi wa Chama cha Umoja Party umemuomba Rais Samia Suluhu Hassan, kuingilia kati kuhakikisha wanapata haki yao ya usajili katika Ofisi za Msajili wa Vyama vya Siasa nchini.
Ombi hilo limetolewa na mwanzilishi wa chama hicho, Seif Maalim Seif aliyesema Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa umekaa kimya na kadri siku zinavyokwenda ndivyo wanavyozidi kuwapatia wakati mgumu kwa kuwa tayari kuna watu wanataka waanze kazi mara moja.
Huyu ndiye mwanzilishi wa chama kipya cha Umoja Party
“Nitumie fursa hii kufanya maombi ya moja kwa moja kwa Rais Samia, yeye ndio mlinzi mkuu wa Katiba na sheria za Tanzania. Kwa taadhima ikimpendeza alitizame suala hili kwa macho mawili.
“Endapo msajili akitoa sababu zake za kutotusajili basi na sisi atufanyie hisani, atuulize na kufanya ‘check and balance’ tujue tatizo ni kitu gani,” alisema Seif.
Onyo kwa chama kipya cha Umoja Party
Aidha, Seif alisema wameamua kutumia picha za hayati John Magufuli katika fulana zenye nembo ya chama chao kwa kuwa falsafa zake na sera zinafanana na alichokuwa akisimamia kiongozi huyo.