Kila baada ya sekunde 40 mtu mmoja mahali fulani hukatisha uhai wake duniani hasa watu wanaokabiliwa na unyanyapaa, kama vile wakimbizi na wahamiaji, watu wa mapenzi ya jinsia moja na wafungwa na mwisho kuchukua maamuzi ya kujiua.
Aidha, watu hawa inawezekana hawana taarifa sahihi ya nini wanapaswa kufanya wakipitia changamoto ya aina hiyo, hivyo kuwa makini endapo utaona dalili zifuatazo kwa mtu kwani ni viashiria kwamba mtu huyo anataka kujiua.
1.Kuweka vitu sawa na kulipa madeni
Hii ni dalili moja wapo ya mtu anaetaka kujiua kwani uanze kupanga vitu ndani ya nyumba na kupanga katika mpangilio mzuri na pia kulipa madeni kwani hataki kuacha madeni mara atakapo kujiua.
2. Kupenda kuongea kuhusu kifo
Kuwa makini na mtu anaependa kuongea kuhusu kifo kwani anakuwa mbioni kutekeleza jambo hilo pia anaweza hata kutumia njia utakazo zitaja bila wewe kujua lengo lake.
3. Kuongea na watu muhimu
Mtu huyu hujaribu kuongea na watu wake muhimu kama njia mojawapo ya kuwaaga na pia kuomba msamaha kwa watu aliowakosea.
Unawezaje kutambua kuwa uhusiano ulionao ni hatari?
4.Tabia ya kulala
Kama mtu anataka kujiua basi hupenda kulala sana kuliko kawaida kwa kufanya hivi kuna mfanya awe pekee yake asijihusishe na mambo mengine anayoona yanampa mawazo na mwisho kuchukua uamuzi wa kujiua.
5. Matumizi ya vilevi
Ongezeko la matumizi ya vilevi kwa mtu huyu huwa kwa kasi sana hasa kama watu wake wa karibu hutumia, hivyo basi kuwa makini na mtu aliyebadilika ghafla na kuanza matumizi ya vilevi.
Hivyo basi endapo utaona dalili mojawapo kwa mtu wako wa karibu jaribu kuongea nae kwa upole na sio kumuhukumu, hakikisha unamtengenezea mazingira mazuri yatakayomfanya ajisikie vizuri na kusahau kabisa wazo lake la kijiua.