Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, amesema Rais Samia Suluhu Hassan, anafanya mambo makubwa kwa taifa na faida yake itaonekana miaka ya hivi karibuni.
Amesema kwa watu wenye upeo wa kuona mbali, wataona namna Rais Samia anavyofanya kazi kubwa.
Akizungumza mbele ya Rais Samia Suluhu jana katika Kata ya Bonga mkoani Manyara, Sumaye alisema wananchi wataendelea kumkabidhi bendera aongoze nchi hadi mwaka 2030.
“Nakuhakikishia kwa niaba ya wananchi , tutaendelea kukukabidhi bendera uongoze nchi yetu hadi mwaka 2025 hadi 2030, haya tunayasema si kwa kukupendelea ni kwa sababu tumeona mambo makubwa unayoyafanya.
“Tunajitahidi sana kuelimisha Watanzania wengine ambao labda upeo si mkubwa kivile, watu wanaangalia hapa karibuni, lakini kwa wale wenye upeo wa kuangalia mbali kidogo kwa nchi yetu, Mama Samia Suluhu Hassan anafanya mambo makubwa kwa taifa hili.” alisema.
Pia alisema wnaanchi wa Manyara, wataendelea kumpa ushirikiano Rais Samia, kwa sababu anafanya kazi kwa Watanzania wa ngazi zote.