Uwekezaji wa bilioni 462 utakavyotoa ajira 7,000

HomeKitaifa

Uwekezaji wa bilioni 462 utakavyotoa ajira 7,000

Kampuni ya Smart Holding kutoka Israel imetangaza mpango ya kuingiza dola milioni 200 (shilingi bilioni 462) katika sekta ya viwanda vya kilimo nchini, uwekezaji ambao unatarajiwa kuajiri zaidi ya watu 7,000.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo, Avi Postelnik amesema wapo kwenye mchakato wa kuandaa mazingira wezeshi ya kuanza kwa mradi huo, ambao idadi kubwa ya wafanyakazi itakuwa ni wazawa.

Amesema kwa sasa wapo kwenye mazungumzo na Chama cha Benki Tanzania (TBA), ili kuunda utaratibu wa kufadhili mradi huo, ambao unajumuisha kupata wafadhili washirika watakaotoa mtaji.

Postelnik amesisitiza kwamba kampuni hiyo pamoja na mambo mengine, itamiliki shamba la ng’ombe wa nyama zaidi ya 2,500, vyakula vya ng’ombe na wengine 1,500 za maziwa zitakazokuwa zinakamuliwa kisasa. Pia kiwanda hicho cha ng’ombe kitahusika pia kutengeneza na kuchakata bidhaa za maziwa.

error: Content is protected !!