Uzembe wa TICTS, hasara kwa taifa

HomeKitaifa

Uzembe wa TICTS, hasara kwa taifa

Kampuni ya kimataifa ya kuhudumia makontena Tanzania katika bandari ya Dar es Salaam (TICTS) imesababishia taifa hasara kubwa baada ya kudondosha makontena matatu baharini na kusababisha meli kushindwa kushusha mafuta kwa siku kadhaa.

Tukio hilo lililotokea wiki iliyopita ni miongoni mwa mlolongo wa tuhuma za uzembe na ukosefu wa ufanisi wa TICTS ambayo imekuwa ikisimamia eneo la makontena la bandari ya Dar es Salaam kwa zaidi ya miaka 20 bila tija.

Njia ya meli kuingia Kurasini kupakua mafuta ilifunguliwa jumatatu baada ya makontena hayo matatu kuopolewa bandarini.

Serikali ya Tanzania kwa sasa iko kwenye majadiliano na TICTS kuhusu kuongeza au kutoongeza mkataba wake, huku kampuni hiyo ikilaumiwa na wadau wa biashara na usafirishaji kwa kukosa ufanisi.

 

error: Content is protected !!