Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro imekuwa hema kwa familia nyingi za jamii ya kimasai ambao huishi humo pamoja na wanyama hao kama ilivyo kwa Wabatwa katika Hifadhi ya Taifa ya Kahuzi-Biega huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Baadhi ya wahifadhi wa hifadhi hiyo ya Kahuzi-Biega wanashikiliwa na polisi kwa kudaiwa kuwavamia na kutekeleza matendo ya kinyama kwa wananchi ndani ya hifadhi hiyo ikiwemo kubaka na kuwaua kwa lengo la kuwafanya wananchi hao waikimbie mbuga hiyo.
Takribani watu 6000 walifukuzwa makazi yao mwaka 1076, miaka sita baada ya kuanzishw kwa hifadhi hiyo na hadi sasa kumekuwa na migogoro ya mara kwa mara.
Wananchi wamejitokeza na kusema kuwa wavamizi na watekelezaji wa ufedhuli huo kuwa ni migambo wa wanyama pori na wanajeshi wa nchi hiyo.
Wabatwa wameamua kurudi kijijini kwao hapo na kusema wana wasiwasi ikiwa watafukuzwa tena hapo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa hifadhi hiyo De-Dieu Bya’ombe Balongelwa amekataa madai hayo katika mahojiano yake na DW na kusema hawajawahi kuwavamia wananchi hao wala hajawahi kuruhusu jambo kama hilo.