Watanzania wanaotaka kuacha pombe wakaribishwa Mirembe

HomeKitaifa

Watanzania wanaotaka kuacha pombe wakaribishwa Mirembe

Taasisi ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe imewataka Watanzania wanaotaka kuacha matumizi ya pombe kwa hiari yao, wakiwemo ambao bado hawajaingia kwenye uraibu, kujitokeza kupata matibabu katika kituo hicho.

Amesema hayo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo, Dkt. Innocent Mwombeki, wakati akipokea dawa hizo zilizoingizwa nchini kupitia Bohari ya Dawa (MSD) na kukabidhiwa kwa taasisi hiyo na Meneja wa MSD Kanda ya Kati, Mwanashee Juma.

Dkt. Mwombeki amesema huduma hizo zitatolewa kupitia Kituo cha Kushughulikia Watu Wenye Uraibu cha Itega, ambapo watapatiwa dawa pamoja na ushauri wa kisaikolojia.

 

error: Content is protected !!