Watu watatu washikiliwa kwa utekaji na mauaji ya mtoto Simiyu

HomeKitaifa

Watu watatu washikiliwa kwa utekaji na mauaji ya mtoto Simiyu

Jeshi la Polisi mkoani Simiyu linawashikilia Yumba Mayala (22), Zakayo Shija (28) na Seba Buchenja (30) wote wakazi wa Malampaka kwa tuhuma za mauaji na utekaji wa mtoto Samike Maleche (5).

Taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi imesema tukio hilo lilitokea Agosti 6, 2026 katika Kijiji cha Gulung’washi, Kata ya Malampaka, ambapo mtoto huyo alidaiwa kutekwa akiwa anachunga mifugo na watu ambao wakati huo hawakuwa wametambulika.

Imeongeza kuwa baada ya mahojiano, watuhumiwa wameeleza kuwa walimteka mtoto huyo ili wajipatie TZS milioni tano kutoka kwa baba yake mzazi, na walipokosa waliamua kumnyonga na kutundika mwili wake juu ya mti ili kupoteza ushahidi.

Aidha, polisi wamesema uchunguzi unaendelea kukamilishwa ili hatua zaidi ziweze kufatwa.

error: Content is protected !!