Wito wa Rais Samia kuhusu uwekezaji wavutia kampuni 400 kutoka Ulaya

HomeKitaifa

Wito wa Rais Samia kuhusu uwekezaji wavutia kampuni 400 kutoka Ulaya

Akiwa kwenye maonesho ya biashara ya kimataifa (Dubai Expo), Rais Samia Suluhu Hassan aliwaalika wawekezaji na wafanyabiashara waliohudhuria mkutano huo kuja kutembelea Tanzania na kujionea fursa za uwekezaji.

Rais Samia alisema ” Nipende kuchukua fursa hii kuwakaribisha nyote nchini Tanzania kwani kuna mazingira mazuri ya uwekezaji na kufanya biashara,”

Hivi sasa kampuni 400 kutoka Umoja wa Ulaya (EU) zinatarajia kuja nchini mwezi ujao kwa ajili ya kuangalia fursa za uwekezaji na biashara kupitia kongamano la biashara na uwekezaji litakalofanyika Februari 23 na 24 mwaka huu, Dar es Salaam.

Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini, Manfredo Fanti amewaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuwa EU ni mshirika mkubwa wa biashara na uwekezaji wa Tanzania ambapo katika kipindi cha mwaka 2021, kiwango cha thamani ya biashara ya EU kwa Tanzania ilikuwa Euro milioni 856 na thamani ya biashara ya Tanzania kwa EU ilikuwa Euro milioni 456.

Alisema katika kipindi cha mwaka 2020, thamani ya uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni (DFI) kutoka kwa kampuni za nchi kumi hai zaidi wanachama wa EU hapa nchini ulikuwa Dola za Marekani bilioni 1.5 kati ya mwaka 2013 na 2020.

“Utafiti uliofanywa mwaka 2021 kwa kampuni takribani 100 za Umoja wa Ulaya zilizoanzishwa hapa ulionesha kuwa wana hisa kwa pamoja za uwekezaji wa takribani Euro milioni 685, lakini tunaamini kuwa Tanzania ina fursa kubwa zaidi za uwekezaji kama inavyothibitishwa na mipango ya kampuni zilizofanyiwa utafiti kuwekeza Euro zaidi ya milioni 250 katika kipindi cha miaka mitano ijayo,” amesema Balozi Fanti.

Kampuni hizo 400 ni miongoni mwa kampuni nyingi zilizoonesha nia ya kutaka kuwekeza na kufanya biashara Tanzania.

error: Content is protected !!