Zainab ammwagia mtu uji Zanzibar

HomeKitaifa

Zainab ammwagia mtu uji Zanzibar

Mkazi wa Mtaa wa Zanzibar, Manispaa ya Musoma, mkoani Mara, Adamu Mohammed ameliomba Jeshi la Polisi limkamate mama mzazi wa mkewe, Zainab Ally kwa madai ya kumjeruhi kwa kumwagia uji wa moto usoni.

Mohamed alidai Novemba, mwaka jana alikorofishana na mkewe, Happiness Moses na kuamua kurudi wao akiwa na mtoto wao wa kiume mwenye umri wa miaka miwili na miezi sita na kusema alikuwa akiwaplekea fehda za matumizi lakini mwishoni mwa Februari mwaka huu alishindwa kuendelea sababu pikipiki aliyokuwa akiitumia kuingizia kipato ilichukuliwa na mmiliki.

“Nimeshindwa kuwahudumia ndani ya wiki kama mbili hivi , mama mkwe na mke wangu walinishtaki ustawi wa jamii, nilijielezea ikaamriwa nijitahidi kwa chochote na mimi niliendelea kuwapelekea nilichokuwa napata,” alisema Mohamed.

Anaendelea kwa kueleza kwamba, Machi mwaka huu yeye na mke wa kaka yake, Restusta Agustino walitumia pikipiki ya rafiki yake kwenda nyumbani kwa mkewe kumchukua mtoto na ndipo alipo mwagiwa uji usoni na mkwewe.

“Shemeji alimfuata Happy baada ya purukushani Happy aliurusha ufunguo, nikasikia mama mkwe akisema ‘ngoja nimuoneshe huyu mbwa’, nilipogeuka nilikutana na uji uliomwagwa na mama Happy,” alisema Restusta.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Zanzibar, Kata ya Makoko, Khamis Fungo alisema alielezwa na mashuhuda wa tukio kwamba kijan huyo hakufanya fujo na kiini cha tatizo kilikuwa Zainab kuchukua fungo wa pikipiki na baadaye kummwagia uji wa moto.

error: Content is protected !!