Malkia wa Uingereza, Elizabeth II ameelezea aliyopitia alipougua Uviko-19 kwa njia ya mtandao wakati wa Uzinduzi wa “Queen Elizabeth Unit” katika Hospitali ya Kifalme Uingereza (Royal London Hospital).
malkia alizungumza na mgonjwa wa Uviko hospitalini hapo Asef Hussain na mkewe ambao walimwelezea kuhusu safari yao katika kipindi hicho kigumu.
Ndipo Malkia Elizabeth II alipoamua kuzungumzia namna naye alivyojisikia akisema kuwa kirusi hicho kilimuacha kiwa amedhoofika na kuchoka na kumwambia Hussain;
“Nimefurahi kuwa unapata nafuu, na [Uviko] inamwacha mtu amechoka sana na kuishiwa nguu, sivyo?Hili janga la kutisha. Sio matokeo mazuri.
“Ni wazi lilikuwa wakati mbaya sana kuwa na COVID kali sana, sivyo?” aliongeza.
Malkia Elizabeth II (95) alipata Uviko mwezi Februari, ambapo inaelezwa kuwa bado alikuwa na nguvu ya kutimiza baadhi ya majukumu yake.